Na
Saleh Ally
SEHEMU
ya tatu nilieleza kuelezea namna ambavyo kulikuwa na baadhi ya mkanganyiko kati
ya kamati ya Taifa Stars na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) wakati wa maandalizi ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Algeria.
Mfano
lile la ndege ya Fastjet na TFF ikaamua kukata tiketi za gharama zaidi huku
ikijua pamoja na gharama kuwa juu, timu ingeondoka bila mashabiki na hata
waandishi wa habari ambao wangekosa unafuu wa safari hiyo.
Hiyo
ilikuwa ni sehemu tu, lakini nakumbushia namna ambavyo niligundua watu walio
nje wanavyotazama Taifa Stars tofauti na wengi walio ndani wanavyoliangalia
suala hilo kwa maslahi zaidi.
Inapofikia
mechi ya Taifa Stars, wengi wanakuwa wanafaidika kama mradi. Wanajua suala la
tiketi lazima kutakuwa na kamisheni, suala la hoteli lazima watapata chao.
Hivyo
mechi moja ya Taifa Stars, inaweza kuwafaidisha watu wengi sana ambao sit u
watakuwa wanaifurahia mechi hiyo kama sehemu ya mafanikio au mapambano kwa
ajili ya taifa letu. Badala yake ni kwa ajili ya faida yao na matumbo yao.
Vitengo
vingi vya utendaji vya TFF, si vile ambavyo watendaji wake ni watu hasa wenye
uwezo wa kusukuma gurumu la maendeleo. Ni watu ambao wako pale kutokana na
utiifu wao kwa uongozi wa Jamal Malinzi.
Hiki
ndicho ninachokiona si sahihi zaidi, ambavyo nilipiga kelele sana kuhusiana na
mshauri wa ufundi wa Rais wa TFF, mtu mmoja hivi aitwaye Bwana Rutta.
Hana
vigezo; hawezi kuwa mshauri wakati yeye anaamini ana uwezo tu wa fitina. Si
mjuzi wa soka, hajawahi kuwa kocha, hajawahi kufundisha hata timu ya ligi kuu.
Sasa anamshauri nini rais wa TFF, haya ndiyo mambo ya kishkaji
ninayoyazungumzia.
Safari
bado si fupi au ndogo kama wengi mnavyoona, kuwa ndani, angalau nikasogea na
kuona TFF wanavyotenda mambo yao kwangu imekuwa faraja kubwa. Sasa ninajua na
nina uwezo wa kuelezea mengi niliyonayo kwa vitendo.
Ningeweza
kwenda mbali zaidi, lakini wakati ninahitimisha mwisho wa makala haya Jumamosi
nitatoa ushauri wangu.
Kingine
ambacho ninaweza kukielezea angalau kwa ufupi ni namna ambavyo TFF iliamua
kuruhusu lundo la viongozi wake kwa Algeria. Wengi hawakuwa na kazi muhimu za
kufanya, sijui walijua Stars itatolewa, kila mtu akataka anaglau asafiri tu ili
‘kufaidi’ mara ya mwisho!
Fedha
walizozitumia maofisa hao, angalau zingetumika katika masuala mengine ya
maendeleo, hata kama ni kununua mipira tu ya watoto, vijana au kazi nyingine
kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini.
Mara
kadhaa, nimesema kuhusiana na Bwana Matandika ambaye mimi bado huwa sielewi
hasa, anafanya nini TFF, kwa nafasi ipi, kazi ipi? Je, inaruhusiwa kikatiba na
nani anayemlipa pale?
Mara
kadhaa, nimekuwa nikiuliza. Lakini naamini kabisa, siku itafika na TFF hili
litawasumbua kwa kuwa ni jambo wanaolichukulia kwa mzaha, lakini fedha
zinazotumika ni mali ya Watanzania kwa kuwa hata kama ni udhamini wa timu ya
taifa basi ni timu ya Watanzania. Fedha zinapaswa kutumika kwa ajili ya timu na
mandeleo ya soka na si kuwapoza washikaji.
Lazima
tukubali, kama tumeamua kuendeleza soka, basi tuwe makini. Mshikaji ambaye
uwezo wake ni mdogo akae kando. Mnakumbuka namna Serikali ya Jakaya Kikwete
ilivyoyumbishwa na washikaji kabla hajaamua kuchenji gia. Haya ndiyo
yanayoukuta TFF kwa sasa.
Sehemu
yangu ya mwisho kabla ya kujumuisha Jumamosi ni kambi ya timu ya taifa ya
Afrika Kusini ambako nilikaa kwa takribani wiki hivi Stars ikijiandaa kucheza
na Algeria mechi ya kwanza Novemba 17 jijini Dar es Salaam.
Kambi
hiyo ilikuwa katika hoteli nzuri na ya kisasa ya Holiday Inn. Hoteli haikuwa ya
kifahari kupindukia, lakini ilifaa kwa kambi na ulinzi ulikuwa mkali. Si lahisi
watu kupita kutokana na ulinzi huo.
Timu
ililazimika kusafiri kwenda kufanya mazoezi takribani kilimita 10 na ushee,
ambalo halikuwa jambo baya kwa kuwa barabara ni bora, usafiri wa uhakika pia.
Kocha
Charles Boniface Mkwasa na benchi lake la ufundi akiwamo mshauri mkuu, Abdallah
Kibadeni, msaidizi wake, Hemed Morocco, kocha wa makipa Manyika Peter walifanya
kazi yao, hakika kwa juhudi kabisa.
Chakula
maalumu cha Kitanzania kiliandaliwa kila siku mchana na usiku. Hakika Kamati ya
Taifa Stars kwa kushirikiana na TFF. Katika hili ninawapongeza, hakukuwa na
kasoro kwao.
Wakati
TFF na kamati walikuwa wamejitahidi katika hili. Makocha walipambana vilivyo,
wachezaji hawakuwa ni wale wenye malengo, waliojitambua au kujua kwa nini wako
pale na nitaanza kwa kuwataka kwa majina na upuuzi waliokuwa wakiufanya.
ENDELEA KUSOMA SEHEMU YA TANO







0 COMMENTS:
Post a Comment