Uongozi wa klabu ya Simba umewaambia ule wa Yanga kama
unataka kumsajili beki wao, Ramadhan Kessy, basi waende mezani kwa ajili ya
kujadiliana nao pamoja na kupanga dau la kumuuza mchezaji huyo ambaye amekuwa
akihusishwa kutakiwa na timu hiyo pamoja na Azam.
Kessy ambaye amebakiza miezi sita ya kuitumikia timu
hiyo ya Simba inayonolewa na Muingereza, Dylan Kerr, ambapo kwa kanuni za
Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa) zinamruhusu beki huyo kufanya mazungumzo
na timu yoyote ile kwa ajili ya kujiunga nayo.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha timu
hiyo, Haji Manara alisema kuwa kama Yanga wana nia ya dhati ya kutaka kumsajili
beki huyo basi wafanye mpango wa kuonana na uongozi wa timu yao kwa ajili ya
kuangalia namna gani wanaweza kumruhusu beki huyo kuhama ndani ya kikosi chao.
“Tunasikia tu kuwa wapinzani wetu, Yanga wapo katika
mchakato wa kutaka kumsajili mlinzi wetu, Ramadhan Kessy jambo ambalo sisi
hatuna taarifa nalo zozote lile kwani wao mpaka sasa hawajaleta barua rasmi ya
kuthibitisha kuwa wana nia ya kumsajili beki huyo.
“Lakini kama itakuwa kweli wanamtaka Kessy basi
tunawaambia waje kuonana na uongozi wetu na kuweka mjadala wa kuangalia
tunaweza kumuuza mchezaji huyo kwa dau gani haswa na kama tukifikia makubaliano
tutamruhusu aende kwani sisi hatuna utamaduni wa kumng’ang’ania mchezaji ila
siyo kumfuata mchezaji huyo kimyakimya wakati wanajua bado ni mali
yetu,”alisema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment