Taifa Stars imepoteza
mechi yake ya kirafiki ya mazoezi dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 23 kwa kufungwa mabao 2-0.
Mechi hiyo
imechezwa kwenye Uwanja wa Eldorado nje kidogo ya jiji la Johanesburg na muda
mwingi vijana hao wanaofundishwa na Shau Bartlet aliyewahi kuchezea Charlton
Athletic ya England na Bafana Bafana walitawala zaidi kipindi cha kwanza kwa
kiasi kikubwa.
Baada ya
mechi hiyo, Kocha Charles Boniface Mkwasa alisema wachezaji wake walicheza kwa
tahadhari kubwa kwa hofu ya kuumia.
"Lakini
kikubwa lilikuwa ni suala la mazoezi na kuangalia makosa ni nini na kipi cha
kurekebisha," alisema Mkwasa.
Baada ya
mechi hiyo, Stars imemaliza rasmi kambi yake ya hapa Afrika Kusini na kesho
inaanza safari kurejea nyumbani.
Kikosi cha Kikosi kilikachoanza leo:
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Haji Mwinyi
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani
6. Jonas Mkude/Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Salum Abubabary/Frank Domayo
9. John Bocco/Elius Maguri
10.Mrisho Ngassa/Malimi Busungu
11. Farid Mussa/Salum Telela
0 COMMENTS:
Post a Comment