Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uganda
‘The Cranes’ Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amemuita mshambuliaji tegemeo
hivi sasa Simba, Hamis Kiiza kwenye kikosi chake.
Timu hiyo, hivi sasa ipo kwenye
maandalizi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika (Afcon) na Kombe la
Dunia 2018.
Kiiza ameitwa kwenye kikosi hicho ikiwa
ni baada ya kuifungia timu yake ya Simba mabao nane hadi hivi sasa katika Ligi
Kuu Bara.
Kiiza
alisema tayari wamepokea barua ya mwaliko wa kujiunga na kikosi hicho pamoja na
beki kisiki wa Simba, Juuko Murshid.
Kiiza alisema, wanatarajia kuelekea kwao
Uganda wakati wowote kuanzia sasa mara watakapotumiwa tiketi za ndege.
“Kikubwa ninashukuru sana kuitwa timu ya
taifa, kwa sababu hiyo inajenga heshima na thamani yangu kwenye klabu yangu ya
Simba.
“Nafikiri nimeitwa timu ya taifa ni
kutokana na uwezo wangu mkubwa niliouonyesha ndani ya uwanja katika ufungaji
mabao na hiyo ndiyo kazi ya mshambuliaji anayotakiwa kuifanya.
“Ninakwenda kujiunga na timu ya taifa
nikiwa nimetokea kwenye majeraha, hivyo nikiwa huko nitaitumikia timu yangu ya
taifa kwa tahadhari kubwa,” alisema Kiiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment