Mwenyekiti wa Chama cha Wanasoka wa Algeria, Ahmed Boudry ameamua kumfungulia mashitaka
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa.
Boudry amesema wamekerwa kupita kiasi na kauli
ya Mkwasa kwamba raia wa Algeria ni wabaguzi wakubwa wa rangi, hivyo
amemfungulia mashitaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
“Alisema
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hata kabla ya mechi ambayo
Tanzania ilifungwa bao saba. Tunaamua kumfikisha Fifa kwa kuwa amewadhalilisha
raia wote wa Algeria wakiwemo wachezaji.
“Hakuwa
na ushahidi, Tanzania imekuja hapa zaidi ya mara moja na hatujawahi kupata
malalamiko ya ubaguzi wa rangi, vipi yeye Mkwasa aseme hayo?” alihoji kiongozi
huyo.
Kabla ya kauli yake hiyo, vyombo vingi vya
habari vya Algeria vilizungumzia suala la Mkwasa kusema Waalgeria ni wabaguzi
wa rangi. Vyombo hivyo vya habari vya Algeria ikiwemo mitandao inayotumia lugha
ya Kifaransa vilimshambuliaji Mkwasa kwa madai amewakashifu Waalgeria.
Algeria iliing’oa Stars kwa kuifunga mabao 7-0
katika mechi ya marudiano mjini Blida ambayo ilikuwa ya kufuzu Kombe la Dunia
2018. Stars imeaga michuano hiyo kwa
kufungwa jumla ya mabao 9-2 kwani awali ilitoka sare ya mabao 2-2 jijini Dar es
Salaam kwenye Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment