Patrick Vieira ameingia mkataba wa kuifundisha New York City FC inayoshiriki
Ligi Kuu ya Marekani maarufu kama Major League.
Mkataba huo mpya kwa Vieira aliyekuwa kocha wa timu ya vijana ya
Manchester City unamfanya kuwa bosi mpya wa wachezaji wengine wakongwe, David
Villa, Frank Lampard na Andrea Pirlo wanaokipiga New York City FC.
Mfaransa huyo aliyeng’ara akiwa na Arsenal anatarajia kuanza kazi rami
Januari Mosi, mwakani.
0 COMMENTS:
Post a Comment