December 16, 2015


Mshambuliaji kindawa Simba, Ibrahim Ajib ‘Cadabra’, ameweka bayana kuwa, hana ndoto ya kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu, badala yake amewaachia Donald Ngoma wa Yanga na Elias Maguri wa Stand United.

Jumamosi, Cadabra alikuwa moto wa gesi katika safu ya ulinzi ya Azam huku akifunga mabao mawili katika sare ya 2-2 na kufikisha mabao matano msimu huu.

Hata hivyo, licha ya idadi hiyo, Cadabra amesema hafungi kuisaka tuzo ya mfungaji bora, muhimu ni kuisaidia timu yake kufika mbali kwani imekuwa kwenye wakati mgumu kwa misimu kadhaa.


“Muhimu ni Simba siyo kusema nang’ang’ania kufunga kuwazia kiatu. Wanaowazia hivyo na wawaze tu, mimi muhimu ni jinsi gani ya kuisaidia Simba kumaliza katika nafasi nzuri mwisho wa msimu. 

"Kama kitakuja mwishoni poa, ila akili yangu ni Simba kwanza, kiatu baadaye nafikiri Donald Ngoma au Maguri wanaweza kukitwaa,” alisema Cadabra, ambaye msimu huu amefunga zaidi ya mabao 10 yakiwemo ya michezo ya kirafiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic