December 16, 2015


Wakati uongozi wa Azam FC ukidai kumuongezea mkataba mshambuliaji wao Mrundi, Didier Kavumbagu, straika huyo amefunguka kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba kwa sasa ndani ya timu hiyo.

Kavumbagu ambaye amekuwa hana furaha ndani ya kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na Muingereza, Stewart Hall, aliomba kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na kukosa nafasi ya kudumu licha ya kucheza michezo mitatu na kuifungia mabao matatu.

“Kiukweli kwa sasa naangalia nawezaje kuisaidia timu yangu kuona inafanikisha malengo tuliyojiwekea kwa sababu suala la mimi kupata nafasi, hilo lipo chini ya mwalimu kutokana na falsafa zake kwani lazima awatumie wachezaji ambao anaamini wanaweza kufiti.

“Suala la kwamba nimeshaongeza mkataba, hilo halina ukweli, inawezakana huyo kiongozi aliyeongea alitaka kujiwekea mazingira mazuri kwa upande wake lakini kwa upande wangu, bado sijafanya mazungumzo na timu yoyote ikiwemo Azam wenyewe kama nitaongeza mkataba, mpaka mkataba wangu utakapokuwa umemalizika,” alisema Mrundi huyo.


Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, ameliambia gazeti hili: “Kavumbagu hatuwezi kumuuza kwa sababu tuna mashindano mbele yetu na tayari tumeshamuongezea mkataba, suala la muda gani itabaki kuwa siri labda aamue kulisema mwenyewe.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic