December 16, 2015


Pamoja ya kusaini mwaka mmoja wa kuitumikia Yanga, straika mpya wa kikosi hicho, Mniger, Issofou Boubacar Garba, pamoja na mwenzake wa Simba, Mkenya, Paul Kiongera, watakosekana kwenye vikosi vya timu hiyo kwenye michezo ya wikiendi hii kutokana na usajili wao bado kutotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mpaka kipindi cha pingamizi kipite. 

Wachezaji hao ambao wamesajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambalo lilitarajiwa kufungwa usiku wa kuamkia leo Jumatano, watalazimika kutozitumikia klabu zao kutokana na Kamati ya Katiba, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF kushindwa kukutana.

Akizungumza, Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema kuwa wachezaji hao wataanza mara baada ya kamati hiyo yenye jukumu la kusimamia mambo ya wachezaji kukutana Desemba 23, mwaka huu kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote waliosajiliwa dirisha dogo.

Kama watapitishwa, maana yake wataanza kucheza katika kipindi ambacho dunia itakuwa ikisherekea sikukuu ya Krismasi.

“Kamati inayosimamia masuala ya usajili wa wachezaji, inatarajia kukutana Desemba 23, kuangalia masuala ya usajili wa wachezaji wote ambao wamesajiliwa kipindi hiki. Baada ya kamati kukutana, ndiyo itatoa ruksa ya kuanza kutumika kwa wachezaji wapya wote,” alisema Kizuguto.


Mbali na Garba na Kiongera, wachezaji wengine watakaokumbana na rungu hilo ni pamoja na kipa mkongwe, Ivo Mapunda (Azam), Brian Majwega, Novatus Lufunga na Hija Ugando (wote Simba), Hassan Dilunga, Khamis Thabit (JKT Ruvu), Tumba Sued (Mbeya City) na wengine wengi.   

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic