Rais
John Magufuli ameamua badala ya kusherekea miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika
tukiwa nyumbani, badala yake, tuingie mitaani na kufanya usafi kupambana na
uchafu ambao umesababisha magonjwa kama kipindupindu.
Wafanyakazi
wa Hoteli maarufu ya Sapphire Court ya Kariako jijini Dar es Salaam nao
waliingia mtaani na kuungana na majirani zao kufanya usafi katika mitaa ya
Kariakoo.
Wafanyakazi
hao wakiwa wamevalia sare zinazoonyesha watu Fulani walio makini, walifanya
usafi kwa zaidi ya saa moja kuanzia eneo la hoteli hiyo hadi nyumba jirani.
Walifanya
usafi barabarani, kwenye mitaro na hata karibu na nyumba za jirani zao na
baadaye wakamalizia katika eneo la hoteli hiyo ambalo halikuwa na kazi kubwa
kwao kwa kuwa inaonyesha limekuwa likifanyiwa usafi mara kwa mara.
MAJIRANI ZAO NAO WALIKUWEPO |
0 COMMENTS:
Post a Comment