Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amecharuka na kumtaka kiungo Justice Majbvi kufunga safari na kuiacha klabu hiyo.
Hans Poppe amesema amekasirishwa na kitendo cha kiungo huyo kukimbilia katika vyombo vya habari bila ya kuutarifu uongozi kwamba ana matatizo.
“Mimi nasema aende zake tu kwa kuwa Simba ina wachezaji wengi sana, hapa Tanzania tuna wachezaji wengi sana.
“Hatuwezi kukubali kupasuliwa kichwa na mchezaji asiyeheshimu mkataba wake. Yeye anadhani vyombo vya habari vinaweza kutatua tatizo lake hilo.
“Basi aende akasaidiwe huko. Tumempa nyumba tatu achague moja, lakini ajabu hajakubali hata moja.
“Nyumba ya Sh laki sita kwa mwezi, nayo hataki. Sasa sisi tufanyeje na mbaya zaidi anakwenda kutudhalilisha kwenye vyombo vya habari,” alisema.
Juzi kuliibuka taarifa mitandaoni ambayo inaelezwa kuandikwa na Majabvi ingawa hata hivyo haijawa na uhakika sana.
Taarifa hiyo ilieleza namna ambavyo maisha ndani ya Simba yasivyo na mpangilio na yamekuwa yakimshangaza kiungo huyo Mzimbabwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment