Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameamua kuweka mambo hadharani baada ya kuonyesha karibu kila kitu ndani ya jumba lake la kifahari.
Ronaldo anaishi katika jumba la kifahari lenye thamani ya pauni milioni 4.8 na liko katika sehemu wanayoishi nyota na mamilionea kibao jijini Madrid.
Jumba hilo liko katika eneo la La Finca ambayo ni sehemu ya kitongoji cha Pozuelo de Alarcon, takribani kilomita 10 kutoka katikati ya jiji la Madrid.
Jirani zake ni ni pamoja na staa wengine ambao ni Gareth Bale na gwiji Mfaransa wa Real Madrid, Zinedine Zidane.
Ronaldo ameamua kuonyesha kila kitu akianzia sebuleni, jikoni hadi chumbani.
Kabla alipita akionyesha mandhari ya nje, ambako kuna uwanja mdogo wa soka, mwanaye Ronaldo Jr, pia kuna uwanja wa mpira wa kikapu na bwawa la kuogelea.

















0 COMMENTS:
Post a Comment