December 22, 2015


Kikosi cha Mwadui FC kiko tayari kwa kazi ya kupambana na Simba na ikiwezekana kuimaliza.

Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri.

“Kufungwa ni sehemu ya mpira, lakini sisi tunataka kufanya vizuri na hayo ndiyo malengo yetu. Hata wale walio mkiani wanataka kushinda,” alisema Julio.
Mwadui FC iko katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 21 wakati Simba SC ina pointi 23 katika nafasi ya nne.


Simba inakwenda Shinyanga baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Jumamosi iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic