December 16, 2015


Yule mwanariadha maarufu wa Afrika Kusini, Caster Semenya amefunga ndoa ya kimila kwa kumuoa mpenzi wake wa kike wa siku nyingi.

Semenya ambaye alikuwa gumzo mwaka 2009 baada ya kushinda mbio za mita 800 jijini Berlin, Ujerumani kutokana na mkanganyiko kuwa ni mwanaume au mwanake, ameamua kufunga ndoa ya kimila.

Hata hivyo Semenya ameviambia vyombo mbalimbali vya habari vya Afrika Kusini kwamba “hajafunga ndoa”.

Mwanariadha huyo amekanusha lakini ushahidi unmahukumu katika ndoa hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita katika jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini.

Semenya anaonekana akiwa amevaa shati la kitenge na jinzi kama mume, huku mpenzi wake wa siku nyingi akiwa amevaa kitenge vizuri kabisa.


Miezi mitatu iliyopita, gazeti moja la Uganda liliripoti kwamba Semenya alikwenda kutoa lobola, yaani mahari na alikuwa katika maandalizi ya harusi.


Lakini Semenya ameendelea kukanusha hilo hilo licha ya ushahidi wa wazi wa picha.

Tokea mwaka 2009, baadhi ya wanariadha hasa kutoka barani Ulaya wamekuwa wakipinga Semenya kushiriki mbio za wanawake wakidai ni mwanaume.

Lakini kumekuwa na taarifa kwamba Semenya ana jinsia mbili lakini mwelekeo zaidi ni upande wa mwanamke.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic