December 23, 2015

PLUIJM

Kikosi cha Yanga kwa sasa kimepungukiwa na wachezaji wengi nyota kutokana na matatizo mbalimbali lakini kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm, amesema hiyo siyo ishu kutokana na upana wa kikosi alichonacho sasa.

Baadhi ya wachezaji hao ambao hawapo kikosini ni pamoja na Mnywarwanda, Haruna Niyonzima aliyesimamishwa na uongozi wa Yanga kwa siku zisizojulikana, Mbuyu Twite aliyekuwa na kadi za njano tatu na kulazimika kuukosa mchezo wa juzi dhidi ya Stand United.
NIYONZIMA

Wengine ni nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Oscar Joshua, Salum Telela ambao wote ni majeruhi wanaosumbuliwa na matatizo ya enka na Malimi Busungu aliyekuwa na matatizo ya kifamilia.

Pluijm alisema kwamba unapokuwa vitani hupaswi kuangalia uliowapoteza, cha msingi ni kutazama uliobakiwa nao na kusonga mbele, hasa unapokuwa na kikosi kipana kama alichonacho kwa sasa ambacho kinamruhusu kuendelea kupambana.

“Ni kweli ninawakosa wengi lakini katika wakati kama huo kwenye mpira unapaswa kuendelea kuwaandaa ulionao na kusonga mbele, hapa nina kikosi kipana na wanastahili kutumika, hivyo ni kuangalia unafanya vipi kuendelea kubaki kwenye mstari sahihi,” alisema Mholanzi huyo.



.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic