December 22, 2015


Klabu ya Azam FC imelia na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwachelewesha kupata leseni kwa ajili ya kukamilisha mjumuisho wa kutoma majina yake katika Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema ameshangazwa na kusikia TFF ikihimiza suala ya utumaji majina Caf kwa kuwa Azam FC ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

“Kawaida lazima TFF itoe leseni kwa klabu, baada ya hapo klabu inaitumia hiyo leseni katika zoezi la utumaji majina.

“Caf haiwezi kupokea majina hayo na kuyadhibitisha kama hauna leseni ya shirikisho. Sasa inashangaza sana kusikia TFF wakituhimiza wakati wanajua hawajatupa leseni,” alisema Kawemba na kuongeza.

“Tumezungumza nao zaidi ya mara moja kuhusiana na suala la leseni na wamehidi kutupatia bila ya mafanikio.


“Sasa tulifikiri wangeanza kukamilisha linalowahusu kwanza halafu watuhimize. Nafikiri si jambo la kiungwana kuamua kwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kusema jambo ambalo unajua wewe ndiye unayelikwamisha,” alisema Kawemba ambaye aliwahi kufanya kazi TFF katika kitengo ambacho anakilalamikia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic