Mshambuliaji
nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefungua hoteli nne alizozipa jina la
CR7.
Hoteli
hizo nne zitakuwa katika miji mitatu tofauti ya
Funchal,
Lisbon nchini Ureno, Madrid nchini Hispania na New York nchini Marekani.
Mradi
huo wa Ronaldo mwenye umri wa miaka 30, utamgharimu pauni milioni 54 kwa wakati
mmoja na zitakuwa chini Pestana Group ambao ni moja ya wataalamu wa masuala ya hoteli kubwa duniani.
Ronaldo
amewaambia waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa hoteli hizo kwamba anajua
hatacheza soka milele.
“Mpira
una muda wake, itafikia wakati sitacheza tena soka. Lakini nitahitaji
kuendeleza maisha kama kawaida, ndiyo maana ninawekeza,” alisema Ronaldo.
SOURCE: DAILY MAIL
0 COMMENTS:
Post a Comment