Mshambuliaji Robert Lewandowski wa Bayern Munich
amekabidhiwa tuzo nne za rekodi maarufu kama Guinness World Records.
Lewandowski amekabidhiwa tuzo hizo baada ya kufunga mabao
matano ndani ya dakika 8 tu wakati Bayern ilipoitwanga Wolfsburg kwa mabao 5-1
katika mechi ya Bundesliga.
Mshambuliaji huyo raia wa Poland aliingia katika mechi hiyo
akitokea benchi wakati huo timu yake ilikuwa nyuma kwa bao 1-0.
Katika tuzo hizo nne za rekodi, zilikuwa zinawakilisha
vipengele hivi; kupiga hat-tick ya haraka zaidi, kufunga bao nne haraka zaidi,
bao tano za muda mfupi na aliyeingia na kufunga mabao mengi.
0 COMMENTS:
Post a Comment