December 1, 2015


Simba imemsajili beki, Novat Lufungo wa African Sports ya Tanga ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.


Taarifa zinaeleza beki huyo wa kati tayari ameishatua mjini Zanzibar na kujiunga na wenzake.

“Kweli Simba imemsajili beki huyo kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, ameungana na wenzake Zanzibar na ameanza mazoezi,” kilieleza chanzo.

Simba iko mjini Zanzibar ambako imeweka kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara ambayo tayari imeanza.


Simba imecheza mechi 9 tayari, iko katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic