Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema ataendelea kumtumia mshambuliaji wake Danny Lyanga kama mshambuliaji wa kati ili kumpa nguvu zaidi ya kufanya vizuri.
Kerr amesema, Lyanga anapaswa kucheza mechi zaidi ili aongeze hali ya kujiamini na kufanya vizuri zaidi.
"Uzuri wa Lyanga ni mchezaji mwenye sifa nyingi, anaweza kufunga au kutoa pasi. Akiendelea kucheza zaidi atapata hali ya kujiamini zaidi na kufanya vizuri.
"Nitaendelea kumtumia kila itakapokuwa inahitajika ili kumsaidia kupata hali ya kujiamini. Akifunga pia itakuwa vizuri maana itamsaidia katika mechi nyingine," alisema Kerr raia wa Uingereza.
Lyanga amekuwa gumzo baada ya kuichezea Simba mechi moja tu dhidi ya Azam FC ambayo aliipeleka mchamchaka.
iungo Azam FC
anunuliwa kwa Sh mil 200







0 COMMENTS:
Post a Comment