Kiungo wa zamani wa
Barcelona na Real Madrid, Luis Figo amesema Cristiano Ronaldo anaweza
kuwashangaza watu na kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
Figo aliyewahi kushinda
tuzo hiyo mwaka 2000 akiwa Barcelona amesema bado Ronaldo ana nafasi licha ya
kuingia fainali dhidi ya Lionel Messi na Neymar, wote kutokea Barcelona.
“Upigaji kura wa tuzo
ni mtu mmojammoja, huwezi kujua mtu kavutiwa na ubora wa mabao au kitu kingine.
“Lolote linawezekana,
Ronaldo anaweza kuwa ndiyo mshindi na watu wengi wakashangaa,” alisema Figo.
Ronaldo ni mshindi wa
Ballon d’Or kwa mara tatu akianza na mwaka 2008 akiwa na Man United, halafu
mwaka 2013 na 2014 akiwa na Real Madrid.








0 COMMENTS:
Post a Comment