Simba inashuka dimbani leo kuivaa Toto Africans katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kocha wa Wekundu wa Msimbazi, Dylan Kerr amesema kuna tatizo katika nafasi ya kiungo ambalo ni Justice Majabvi.
Wakati Simba ikiwa jijini hapa kwa mchezo huo, Majabvi raia wa Zimbabwe amebaki Dar es Salaam akishughulikia mgogoro na uongozi akitaka kufuatwa kwa baadhi ya vipengele vya mkataba wake ikiwemo malazi mazuri.
Kerr raia wa Uingereza amesema hajafurahishwa na Majabvi kutojiunga na timu yake hivyo ameutaka uongozi kumaliza tatizo lake haraka ili amtumie.
“Majabvi ni mchezaji muhimu kikosini na nasikitika kumkosa, ili ni pengo kwetu lakini hatuna jinsi tutapambana na wachezaji waliopo ili tufanye vizuri,” alisema Kerr.
“Uongozi unapaswa kumaliza tatizo lake haraka ili aje kuitumikia timu kwani kumkosa ni pigo kubwa sana kwangu.” Kutokana na kukosekana kwa Majabvi, Kerr atapaswa kumtumia Jonas Mkude katika nafasi yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment