December 19, 2015


Kutokana na kufanikiwa kuwasajili Brian Majwega, Paul Kiongera na Danny Lyanga, straika Hamis Kiiza wa Simba amesema kikosi chao kimebadilika na sasa kina mwonekano mpya wa ushindi.

Majwega ni kiungo mshambuliaji kama ilivyo kwa Kiongera wakati Lyanga ni straika, wengine waliosajiliwa na Simba wakati huu ni beki Novatus Lufunga wa African Sports na straika Hija Ugando.

Kiiza raia wa Uganda aliyewahi kuichezea Yanga, amejigamba kuwa ujio wa wachezaji hao utaiongezea nguvu Simba na anaamini pia utamuongezea kasi ya ufungaji.

Hadi sasa Kiiza amefunga mabao nane sawa na Donald Ngoma wa Yanga wakati straika wa Stand United, Elias Maguri akiongoza kwa kufunga mabao tisa katika mechi 11.

Alisema Simba sasa inakuja kivingine kwani usajili uliofanywa umezingatia mahitaji ya timu na mashabiki wategemee mambo mazuri kutoka kwao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic