December 16, 2015


Baada ya kutoa pasi ya bao na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na Mbeya City, kocha mkuu wa timu hiyo, Meja Abdul Mingange, amesema Haruna Moshi ‘Boban’ ni kiungo hatari sana.

 Boban juzi alifanikiwa kuifungia timu yake bao la kusawazisha kwenye mchezo waliotoka sare ya mabao 2-2 dhidi Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kocha ambaye ni Mwanajeshi mstaafu amesema kwa kiasi kikubwa Boban kwa sasa amebadilika na anafanya vizuri kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi.

“Boban kwa sasa yupo vizuri, ni wazi inaonyesha kweli ameamua kutulia na kucheza mpira, juhudi zake zinaonekana licha ya kupitia changamoto kadhaa za kisoka kama ilivyokuwa kwa mwenzake, Juma Kaseja.

“Kwa sababu anabadilika kila kukicha tofauti na pale tulipoanza naye kama kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa alicheza vyema, akatoa asisti ya bao na baadaye alifunga bao la kusawazisha licha ya kucheza na timu ambayo ina uzoefu mkubwa na tunaiheshimu,” alisema Meja.

Ikumbukwe Boban aliwahi kukipiga Simba kwa mafanikio na baadaye akaondoka kwenda Coastal Union, hakumaliza msimu akavurugana nao akawa hana timu na mwisho wa siku akatua Friends Rangers.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic