Beki kisiki wa Simba, Juuko Murshid ameungana na wenzake na kuanza mazoezi.
Juuko ameungana na Simba inayojiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara kesho dhidi ya Azam FC.
Beki huyo alikuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda alichokisaidia kubeba ubingwa wa Chalenji katika michuano iliyofanyika nchini Ethiopia.
Beki huyo Mganda wa Simba, leo amefanya mazoezi pamoja na wenzake kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM).







0 COMMENTS:
Post a Comment