December 21, 2015


Kufungiwa miaka nane kwa Rais wa Fifa, Sepp Blatter na Rais wa Uefa, Michel Platini ndiyo jambo gumzo zaidi mitandaoni kwa sasa.

Blatter na Platini, kila mmoja amefungiwa miaka nane kujihusisha na masuala ya mpira.

Wawili hao wamefungiwa na kamati ya nidhamu ya Fifa jijini Zurich, Uswiss leo hii.

Hali hiyo inamfanya Blatter akae nje ya soka na huenda ndiyo mwisho wake wakati Platini raia wa Ufaransa na gwiji la soka barani Ulaya enzi zake, hataweza kugombea Urais wa Fifa utakaofanyika Februari 26, mwakani.


Sehemu mbalimbali katika mitandao wanajadili kuhusiana na adhabu ya magwiji hao katika uongozi kisoka, duniani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic