![]() |
| UHURU |
Nyota wa Tanzania wanaokipiga nchini Afrika Kusini ‘Sauz’, Mrisho Ngassa na Uhuru Selemani wamerejeshwa nchini na timu zao kwa ruhusa maalumu.
Ngassa aliyewahi kuzitumikia Yanga, Azam na Simba kwa sasa anakipiga Free State Stars ya Ligi Kuu ya Sauz lakini Uhuru aliyewahi kuwika akiwa Simba kabla ya kutua Azam yeye anaichezea Royal Eagles ya Ligi Daraja la Kwanza kwa mkopo akitokea Jomo Cosmos.
Uhuru yupo Dar wakati Ngassa yupo Arusha ambapo ruhusa hiyo ni kutokana na Sikukuu ya Krismasi ambapo michuano mbalimbali nchini humo ikiwemo ligi za soka zimesimama kwa ajili ya kupisha sikukuu hiyo.
“Nitakuwepo kwa muda tu, maana ligi kule zimesimama na tumepewa ruhusa ya kama wiki moja tu, nafikiri nitaondoka Desemba 26 au 27 maana mazoezi yanatarajia kuanza Desemba 28,” alisema Uhuru.
Upande wa Ngassa alisema: “Nipo zangu Arusha na familia kwa ajili ya Krismasi kisha baada ya hapo nitarudi Sauz kuendelea na majukumu kama kawaida.”
Kulikuwa na taarifa kuwa Ngassa alirejea nchini kutokana na kuwepo kwa mgogoro wa kifamilia unaohusu wazazi wake lakini yeye mwenyewe amekanusha madai hayo.








0 COMMENTS:
Post a Comment