December 13, 2015


Huyu jamaa anaitwa Danny Lyanga, aliwahi kuichezea Coastal Union kabla ya kuondoka nchini ya kwenda DR Congo kukipiga FC Lupopo.

Sasa yuko Bongo tena anakipiga Simba na jana aliichezea kwa mara ya kwanza wakati ikipambana na Azam FC, kazi yake imekuwa gumzo licha ya kwamba mechi iliisha kwa sare ya bao 2-2 na Lyanga hakufunga.

Lakini uwezo aliouonyesha, kasi, upigaji mashuti,  Lyanga alionyesha mambo mengi kwamba ni mshambuliaji hasa. Kama ataendelea hivyo, basi Simba ina nafasi ya kurudisha heshima.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic