December 25, 2015


Ili kuhakikisha wanakabiliana na hali ya hewa ya mvua inayoendelea katika viwanja vya mikoani, wachezaji wa Simba wamepatiwa viatu vya mvua ili kukabiliana na hali hiyo.

Simba ambayo ilitoka sare katika mchezo dhidi ya Toto Africans, wiki iliyopita ambapo katika mchezo huo kulikuwa na mvua, iliyosababisha mchezo huo kupoteza mvuto, pia inatarajia kuvaana na Mwadui FC, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally 'Gasgoine', amefunguka kuwa kwa sababu kipindi hiki ni cha msimu wa mvua, viwanja vingi vinakuwa katika hali mbaya, ndiyo maana uongozi umeamua kuandaa viatu maalumu kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo ili wachezaji waweze kuvitumia.

“Tumejiandaa ipasavyo kuhakikisha tunashinda mchezo wetu dhidi ya Mwadui pamoja na mechi zote zilizo mbele yetu, kwani kila mechi kwetu ni fainali.


“Kuhusu mvua ndani ya siku mbili hizi imekata ila ilinyesha juzi kidogo na mwalimu anarekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Toto katika kila idara ili kurejesha hali ya timu. Viatu hivyo vitatusaidia kupambana popote pale patakapokuwa na mvua,” alisema Abbas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic