| KIONGERA |
Uongozi wa Simba umejiandaa vilivyo kuhakikisha mchezaji wake mpya, Paul Kiongera raia wa Kenya anaishi katika mazingira mazuri ili afanye kazi yake vizuri.
Nyota huyo ambaye alirejea kikosini wiki mbili zilizopita akitokea KCB ya Kenya alipokuwa kwa mkopo, hata hivyo mpaka wikiendi hii alikuwa hajajua pa kuishi kutokana na kuwa kambini tangu amejiunga nao huko Zanzibar kabla ya kuweka kambi huko maeneo ya Changanyikeni, Dar kujiandaa dhidi ya Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’, amesema, suala la Kiongera ataishi wapi hawana presha nalo kwani tayari kuna nyumba tatu zilizo wazi, hivyo ni yeye kuchagua aishi wapo na nani.
“Kuna nyumba tatu pale Shekilango zipo wazi mpaka sasa, atachagua mwenyewe aishi wapi na akina nani. Mfano kuna sehemu alikuwa anaishi Simon Ssserunkuma, bado haina mtu akipenda atahamia hapo,” alisema Gazza.
Awali, straika huyo kipenzi cha Wanasimba, alikuwa akiishi Chang’ombe lakini kwa sasa nyumba hiyo ina watu wengine, akiwemo daktari wao, Yassin Gembe.







0 COMMENTS:
Post a Comment