![]() |
| VAN GAAL AKIINUKA NA KUONDOKA KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUUENDESHA KWA DAKIKA 4 NA SEKUNDE 58 TU. |
Louis van Gaal sass mambo yanaonekana kumshinda England.
Maana amejikuta akiinuka na kuondoka wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika klabu ya Manchester United.
Van Gaal alilazimika kufanya hivyo baada ya kuulizwa anazungumziaje suala la kutemwa iwapo atafungwa na Stoke City na nafasi take ichukuliwe na Jose Mourinho.
Wakati mkutano huo wa waandishi ulikuwa umefanyika kea dakika 4 na sekunde 58, van Gaal aliinuka na kuondoka, huku akisema “tutaonana mwakani.”
Akikiongoza kikosi cha Man United, kimepoteza mechi tatu mfululizo na kukifanya kionekane kuwa taabani naye si mkombozi kama ilivyozoeleka.
Sasa Kocha Mourinho ambaye yuko huru baada ya kutemwa na Chelsea ndiye anapewa nafasi kubwa ingawa makocha wengine kama Pep Guardiola wanatupiwa macho na Manchester United.









Aina hii ya uandishi wa habari nachoka nayo kabisa,
ReplyDeleteukiangalia ile clip na jinsi alivyokuwa anaongea, si kwamba amekimbia Waandishi, Van Gaal anaonyesha jinsi masikitiko yake yalivyo kutokana na media ilivyoandika kuhusu kufutwa kwake kazi, kwa hiyo anahisi hana cha kuongelea kuhusu hizo rumours, na akasema yupo hapo kwenye hiyo press conference kwa sababu ya sharia za Premeir League kwamba lazima u address media kabla ya game lakini isingekuwa hivyo maana yake asingefanya press.
Kwa wazungu kuna tamaduni tofauti, ndio maana hata Wenger anasema kwamba ni kama kumkosea heshima Van Gaal, lakini huwezi kuzuia Waandishi habari kufanya hivyo hasa kwa timu kubwa zinapokuwa na matokeo mabaya.....
Lakini na nyinyi Waandishi wa habari wa bongo mnapoandika habari za Ulaya, muwe mnafanya kwa weledi wa juu.
Binafsi nimeoiona ile clip, lakini kilichoandikwa hapo juu hakiendani kabisa na ile clip..
Mantiki ya VAN GAAL, ni Waandishi kumdharaulisha kuhusu kufutwa kazi, ni kitu ambacho toka mechi ya Norwich kimesemwa sana, sasa kwa wenzetu si heshima na yeye kama Van GAAL amekasirishwa ni kitendo hicho, kwa hiyo kasema anachoweza kuongea ni kuhusu mechi ya Stoke tu, na kwamba amefanya kila linalowezekana ili kuongeza uwezo wa kujiamini, na kurudisha morali ya timu....sasa Waandishi walitaka zaidi kuhoji kuhusu kufukuzwa kwake kuliko mechi yenyewe, ndio maana akawaaga kwa kuwaambia heri ya X-mas na Mwaka Mpya.....!