December 24, 2015



Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema kiungo mkongwe wa Simba, Mwinyi Kazimoto ni muhimu sana katika kikosi chake.

Kerr amesema Kazimoto ni kati ya wachezaji wenye msaada mkubwa na asitokee mtu akamdharau kwa kuwa haanzi katika mechi nyingi.

“Kazimoto ni muhimu, ni mchezaji anayeweza kuwaongoza wenzake lakini amecheza nje ya Tanzania. Hivyo anaweza kuwa na mengi ya kuchangia katika timu kutokana na alivyojifunza,” alisema Kerr.

Awali kulikuwa na taraifa kwamba Kerr raia wa Uingereza haridhishwi sana na kiwango cha kiungo huyo ambaye alijiunga na Simba akitokea Al Markhiya ya Qatar.


Kazimoto ambage alichipukia kisoka kwao mkoani Mwanza alitokea Simba kujiunga na timu hiyo ya Qatar, lakini baada ya kurejea Simba Al Markhiya ilitangaza kutaka kumsajili tena, lakini ikashindikana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic