December 11, 2015


Mwanasoka wa Honduran, Arnold Peralta amepigwa risasi na kuuwawa katika mji wake wa nyumbani.
Peralta amepigwa risasi akiwa katika maegesho ya magari katika eneo la maduka na aliyemuua bado hajajulikana hadi sasa.

Kiungo huyo ,26’ aliyewahi kuichezea Rangers ya Scotland hadi Januari mwaka huu, ameuwawa katika eneo ambalo limekuwa likiaminika kuwa na mauaji mengi ya watu yaliyotawaliwa na visasi.


Peralta amewahi kuichezea Honduras katika michuano mbalimbali ya kimataifa na wachezaji wa Rangers watatoa heshima ya dakika moja na kuvaa vitambaa vyeusi katika mechi yao ya wikiendi hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic