December 1, 2015



Dar es Salaam, 1st December 2015, Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga  amerudi nchini kutoka Marekani alipoenda kwa ziara ya wiki moja kwaajili ya kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuziki nguli Akon

Nalimi Mayunga alisema hii imekuwa nafasi ya pekee maishani mwake  na anapenda kuwashukuru sana Aitel na Trace kwa kupatia fulsa hii.

“Nimefurahia muda niliokaa mjini Losa Angeles Marekani na kupata wakati mzuri wa kumtembelea Akon nyumbani kwake na kufanya rekoding ya video na kupata mafunzo ya musiki alisema.

Nalimi aliongeza kwa kusema fursa hii imenipa mwanga zaidi  katika namna ya kufikiri na kujipanga ili kuzifikia ndoto zangu katika tasinia ya muziki.  Nimejifunza mambo mengi sana kupitia mafunzo niliyopata kutoka kwa Akon ikiwemo jinsi ya kukabili jukwaaa, namna ya kuchezea sauti yangu, mafunzo ya sauti,  namna ya kuandika na kutunga nyimbo na jinsi ya kuinua muziki wangu na kukuza kipaji changu kwa
ujumla.”



Nalimi aliyejawa furaha pia alieeleza shauku aliyonayo ya kutoa kibao hicho kwa kushirikiana na Akon na kusema kwamba kitafungua milango yake katika ulimwengu wa muziki kwani amepata nafasi ya kuingia na kurekodi wimbo wake kwenye studio ya universal Hollywood yenye vifaa
vya kisasa na vyenye technologia ya juu na uhakika video yangu itakuwa moja kati ya video bora za muziki
sokoni na hivyo nawashurukuru sana mashabiki wangu, watanzania  kwa ujumla kwa kunipigia kura na kuniwezesha kufika hapa nilipo leo.”

Akieleza zaidi kuhusu safari ya Mayunga, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya alisema “  tunafurahi kuwa sehemu ya kubadilisha maisha ya vijana wengi akiwemo Nalimi Mayunga. Tunaamini mayunga atakuwa ni mfano utakaowavutia vijana wengi kuzifikia ndoto
zao. Tunapenda kuwahamasisha vijana wengi zaidi kushiriki katika program zetu nyingi zenye lengo la kuwawezesha kufikia malengo yako kama vile Airtel Fursa, Airtel Rising Stars, Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi.



Msimu wa pili wa shindano kubwa la muziki la Afrika  la Airtel Trace 
Music Stars mwaka 2016 linategemea kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa January 2016, tunatoa wito kwa vijana wengi kushiriki pindi shindano hili litakapotangazwa rasmi," aliongeza Mallya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic