Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’
kinatarajiwa kuwasili kesho mchana jijini Dar ess alaam kikitokea nchini
Ethiopia kilipokuwa kinashiriki michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za
Afrika Mashariki na Kati.
Kilimanjaro Stars imetolewa katika hatua ya robo fainali na
wenyeji Ethiopia kwa mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika
dakika 90 za mchezo huo, na wenyeji kushinda kwa penati 4-3.
Timu ya
Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni na msaidizi wake Juma
Mgunda, iliongoza kundi lake katika hatua ya makundi kabla ya kukutana na
wenyeji Ethiopia katika mchezo wa robo fainali.
Katika michezo wa
makundi, Kilimanjaro iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Somalia, ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, na sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia.
Baada ya kurejea
nyumbani, TFF kwa kushirikiana na benchi la ufundi wataanza maandalizi ya
michezo dhidi ya Chad itakayochezwa Machi 2016 kuwania kufuzu kwa Fainali za
Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017.







0 COMMENTS:
Post a Comment