Mshambuliaji Paul Nonga wa Mwadui FC, tayari yuko jijini Dar es Salaam tayari kumalizana na Yanga.
Nonga aliyewahi kung'ara akiwa na Mbeya City ametua Dar es Salaam ili kumalizia makubaliano na Yanga, iwapo watakubaliana, leo atamalizana na Yanga kwa kuwa ndiyo siku ya mwisho ya dirisha dogo.
"Kweli yuko Dar na kwa mazungumzo, nafikiri wamefikia hatua ya mwisho na viongozi wa Yanga.
"Kimebaki kitu kimoja tu, ni suala la malipo na masharti fulani hivi kidogo. Wakikubaliana, basi anasaini," kilieleza chanzo.







0 COMMENTS:
Post a Comment