December 25, 2015




Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameamua kuwa atampa nafasi ya kutosha mshambuliaji wake mpya, Paul Nonga na baada ya hapo, mpini utakuwa mkononi mwake.

Nonga ataamua mwenyewe kwamba amuonnyeshe Pluijm kuwa anahitaji nafasi ya kuendelea kupangwa au la na mambo yote yatakuwa kwa vitendo.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kwamba, Pluijm ameridhishwa na uwezo wa Nonga na angependa kutoa nafasi kwake mapema.

“Inaonekana kocha amemkubali na anataka ampe nafasi mapema na mwenyewe itakuwa kazi kwake kuonyesha ana tanki lenye mafuta kiasi gani.

“Unajua tokea alipocheza mechi ile ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers, kocha ameonekana kumfurahia sana,” alisema.


Katika mechi hiyo dhidi ya Friends, Nonga alifunga mabao mawili huku Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic