December 30, 2015


Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm mpango wake mpya alionao sasa ni kujaribu kuwapa nafasi na kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu Bara.

Lakini mkakati huo utaanza kutumika kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza rasmi Januari 2, mwakani huko visiwani ikiwemo kuendelea kuangalia zaidi kasi za wachezaji wapya waliosajiliwa kikosini humo hivi karibuni.

Pluijm amesema kuwa nia yake ni kushindana lakini pia itakuwa ni fursa nzuri kuwapa nafasi vijana wengine wakiwemo wale waliopandishwa hivi karibuni wakitokea kikosi cha timu ya vijana maarufu kama Yanga B.

“Tutakwenda kupambana kama ilivyo kawaida huwezi kusema kwamba utachukua ubingwa kama hutaweka nia ya kufanya vizuri kwenye michezo ya awali, hivyo tutatumia ushindi wa kila mchezo ili kufikia hapo tunapopataka.

“Lakini pia itakuwa fursa nzuri ya kuangalia vijana wengine ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kutosha kwenye ligi na michuano mingine nao kutumika na kuonyesha zaidi, taratibu kutakuwa na mchanganyiko lakini nia ni watu kupata nafasi pia.

“Kwenye kundi letu tupo na Azam, Mtibwa pia, tunatoka ligi moja lakini kwenye mashindano haitakiwi kuogopa kitu, tutakutana nao na nia yetu ni kushinda,” alisema Pluijm aliyeiongoza Yanga SC kutwaa ubingwa wao wa 25 msimu uliopita.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic