December 30, 2015


Baada ya kuonekana kusuasua katika michezo kadhaa iliyopita hatimaye beki wa Azam, FC Muivory Coast, Pascal Wawa, amefunguka kuwa kiwango chake kimeporomoka kwa kasi ya ajabu kutokana na ligi kusimama mara kwa mara.

Beki huyo ambaye kwa sasa ni msimu wake wa pili ndani ya Ligi Kuu Bara amekuwa na nafasi ya kudumu ndani ya kikosi hicho, huku akisifika zaidi kwa mtindo wake wa kucheza kwa kujiamini.

 Hata hivyo, Azam tayari imecheza mechi mbili toka itoke mapumziko ambapo dhidi ya Simba walitoka sare ya 2-2 na ikiichapa Majimaji mabao 2-1.

Wawa amesema sababu kubwa iliyopelekea kushuka kwa kiwango chake katika mechi za hivi karibuni kimwango chake ni kutokana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusimamishwa ligi mara kwa mara.

“Kiukweli katika hizi mechi mbili ambazo tumecheza mpaka sasa siwezi kupinga kama nimecheza chini ya kiwango ni kweli lakini hii inatokana na ligi kusimamishwa mara kwa mara hali ambayo inaathiri viwango wa wachezaji wengi.


“Ligi inasimama kwa muda mrefu na wachezaji tunalazimika kurejea majumbani mazoezi tunafanya lakini shida inakuja kwa sababu kunakuwa hakuna mashindano yoyote na hii inachangia kutufanya kipindi cha mwanzo tunaonekana kupotea ila ninaamini kabla ya mashindano ya kimataifa nitakuwa fiti,”alisema Wawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic