Baada ya ligi kusimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa kwa sasa ni ruksa wachezaji wake kwenda mapumziko.
Mwadui ambayo inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 22 nyuma ya Simba ambao wana alama 24, ikiwa ni msimu wake wa kwanza baada ya kushuka miaka kadhaa iliyopita mchezo wake wa mwisho ilitoka sare ya bao 1-1 na vijana hao wa Msimbazi.
Ikumbukwe timu hiyo tayari imevaana na vigogo wa ligi ambao ni Yanga, Azam na Simba na Azam pekee ndiyo iliibuka na ushindi huku wengine wote wakiambulia sare.
Kocha huyo amesema kwa sasa ni muda wa mapumziko ndiyo maana kaamua kuwapa nafasi wachezaji wake kula bata ili ukifika muda wa kazi wote wawe tayari.
“Ligi inasimama lakini wachezaji wangu nimewaacha tu wapumzike bila tatizo, sitaki kuongeza programu zozote kwa sasa lakini ukifika muda wa kurejea kazini kweli wanatakiwa kufanya kazi kwa sababu kama ni uhuru nitakuwa nimewapa wa kutosha,” alisema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment