December 23, 2015


Baada ya kukaa chini na kuiangalia kwa umakini safu ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na Danny Lyanga na Hamis Kiiza, Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameibuka na kusema hatishwi hata kidogo na wapinzani wake hao.

Julio na kikosi chake cha Mwadui kinatarajiwa kuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utakaopigwa wikiendi hii katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani wa hali juu kutokana na ukaribu uliopo baina ya timu hizo kwenye msimamo wa ligi.

Julio ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa hatishwi hata kidogo na kasi ya upachikaji mabao ya safu hiyo ya Simba kwa kuwa tayari ameshawaandaa mabeki wake kuhakikisha wanakabiliana vilivyo na washambuliaji hao.

“Hawa washambuliaji wa Simba kina Kiiza (Hamis), Kiongera (Paul) na Lyanga (Danny), kwa hakika sina hofu nao hata kidogo kwani tayari nishawapa mbinu mabeki wangu za kuwazuia na nina uhakika watalifanya jambo hilo kwa ustadi mkubwa.


“Lakini vilevile nilikuwa nataka kuwaambia kuwa waje katika mchezo huo wakiwa wameweka akilini mwao kuwa ni lazima waziache pointi tatu hapa kwani kwa sasa tuko vizuri na wachezaji wangu wote wanaonyesha uchu wa kutaka kushinda kila mechi,” alisema Julio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic