December 24, 2015


Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall ameagiza beki wake, Aggrey Morris kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua kinachomsumbua.

Morris amekuwa majeruhi sasa kwa zaidi ya wiki mbili jambo ambalo limefanya kocha huyo Mwingereza aamue afanyiwe vipimo zaidi na sahihi.

“Nahitaji kuona vipimo vya uhakika ili tujue hasa kinachomsibu na kama litakiwa suala la matibabu basi lifanyike ili arejee uwanjani,” alisema Hall alipozungumza na Salehjembe.

Hall amesema suala la majeruhi mfululizo limekuwa likimuathiri katika mechi nyingi na sasa ameamua lishughulikiwe kwa kina.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic