December 24, 2015


Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema yeye ndiye alizuia mchakato wa Azam FC kuachana na beki wake wa kati David Mwantika.

Hall amesema baada ya kumalizana na Azam FC katika suala la kurejea klabuni hapo, alikuta taarifa kwamba imeamua kuchana na Mwantika.

“Nilitaka kujua kwa nini Mwantika anaachwa, lakini nilipofuatilia niligundua kiwango chake bado ni kizuri. Niakazuia asiachwe na suala lake lishughulikiwe.

“Mwantika bado ni beki mzuri na atakuwa msaada tu kwa Azam, ninaamini ni sehemu ya mabeki bora hapa nchini na akipata nafasi ya kucheza ataonyesha hicho,” alisema.


Baada ya Azam FC kuwa katika mchakato wa kuachana Mwantika, Simba ikaamua kumfuatilia na mazungumzo yakafanyika lakini ikashindikana katika hatua za mwisho kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic