December 1, 2015

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI (WA PILI KULIA) AKIONGOZA MKUTANO MKUU ULIOPITA MJINI MOROGORO, KULIA NI KATIBU MKUU WA TFF, SELESTINE MWESIGWA.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kufanya mkutano wake Mkuu wa Mwaka kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo wajumbe wa mkutano huo tayari walishatumiwa taarifa za mkutano.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF, Kaimu Mkurugenzi wa Sheria na Wachama, Elliud Mvela amesema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri.
Mvella amesema ajenda za mkutano mkuu wa kawaida ni zile zilizopo kikatiba, ila itaongezeka ajenda ya marekebisho ya katiba ambayo ni mapendekezo yaliyotolewa na FIFA.
Agenda za mkutano mkuu ni:
1.Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa Wajumbe
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita.
5. Yatokanayo na Mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Ripoti kutoka kwa Wanachama
8. Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
 9. Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
10. Kupitisha bajeti ya 2016
11. Marekebisho ya Katiba
12. Mengineyo

13. Kufunga Mkutano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic