Hatimaye Gary Neville amepata ushindi wa kwanza akiwa kocha wa kikosi cha kwanza.
Neville ndiye Kocha Mkuu wa Valencia ya Hispania na ameingoza timu hiyo kuitwanga Barakaldo mabao 2-0 katika mechi ya michuano ya Copa del Rey.
Ushindi huo dhidi ya Barakaldo umeivusha Valencia hadi hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ya Copa del Rey.
Neville ambaye msaidizi wake ni mdogo wake wa damu, Phil Neville alianza kazi yake kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Lyon katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kipigo hicho kimewang’oa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa watacheza Europa Cup.
0 COMMENTS:
Post a Comment