Kiungo wa zamani wa Simba, Shekhan Rashid ametimiza miaka mitano ya ndoa yake.
Yanga imecharuka kuhusiana na kiungo wake Haruna Niyonzima kuonyesha dharau kwa uongozi na wanachama wa klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amezungumza na SALEHJEMBE na kusema wamekuwa hawafurahishwi kwa muda muda mrefu sasa kutokana na tabia za Niyonzima za kuchelewa kila anapokwenda Rwanda.
“Niyonzima amekuwa na tabia si nzuri kwa maana ya nidhamu kila anapokuwa kwao Rwanda. Mfano tumemruhusu kwenda kuitumikia Rwanda katika michuano ya kimataifa, hadi sasa hajarejea.
“Angalia mchezaji wa Azam FC kama Mugiraneza ambaye anacheza timu moja na Haruna ameisharejea, wachezaji wa Simba waliocheza fainali wako katika klabu yao.
“Niyonzima hajarejea na wala hasemi lolote. Si Jambo sahihi na hili linaonyesha tabia isiyo sahihi kwa maana ya kuheshimu majukumu yake katika klabu,” alisema Dk Tiboroha.
“Haruna amekuwa akifanya hivi mara kwa mara, lakini sasa tumechoka na kama tutachukua hatua kali, basi wanachama wajue kabisa mapema.
“Tumekuwa tukitoa adhabu kwake mara kadhaa, lakini mambo hayabadiliki. Wakati mwingine tumemkata mshahara hadi sasa tunaona kama tumechoka, lakini mambo ni yaleyale.”
.








0 COMMENTS:
Post a Comment