December 22, 2015


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Paul Nonga amesema anajua Yanga ina kikosi kipana, lakini anataka kucheza kikosi cha kwanza.

Nonga amesema anajiamini atatoa ushindani na msaada kwa kikosi hicho kwa kushirikiana na wenzake.

“Nataka kucheza kikosi cha kwanza, haitakuwa kazi rahisi lakini nitajituma na kufanya kazi kwa ufanisi.
“Ushindani unaoleta tija ni sehemu ya maendeleo, nitashindana nipate namba ili niwe sehemu ya msaada kwa kikosi,” alisema Nonga.


Nonga amejiunga na Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili akitokea Mwadui FC. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic