December 12, 2015


Siyo siri kwamba Yanga imemtema makusudi kiungo Mbrazili, Andrey Coutinho ili ipate nafasi ya kumsajili Issofou Boubacar raia wa Niger, tayari klabu hiyo imempa jezi namba 14 iliyokuwa inavaliwa na Joseph Zuttah.


Tukio hilo limetokea katika hali ya kushangaza kwani bado Boubacar ambaye ni straika hajasaini mkataba wa kuichezea Yanga badala yake anafanya mazoezi tu na kikosi cha kwanza.

Ili kuonyesha kwamba ni lazima asajiliwe kabla ya kufika saa 6:00 usiku wa Desemba 15, mwaka huu, Yanga imembeba Boubacar na ipo naye jijini Tanga ambapo leo inacheza na Mgambo Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tumempa Boubacar jezi hii kutokana na kuwa ndiyo iliyobaki kwa sasa kikosini na ndiyo iliyokuwepo kwa karibu.”
Jezi namba 14 imewahi kuvaliwa pia na Omega Seme ambaye hakuwa na kipindi kizuri kikosini, pia Zuttah aliachwa muda mfupi baada ya kusajiliwa.


Wachezaji wengine wa kigeni wanaocheza Yanga ni Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite (wote Rwanda), Vincent Bossou (Togo), Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma na Thabani Kamusoko wa Zimbabwe

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic