December 12, 2015


Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema atampa jukumu la kupiga penalti mchezaji yeyote wa Simba lakini siyo kiungo Jonas Mkude.

Mkude ameponzwa na penalti aliyokosa wakati akiichezea Kilimanjaro Stars katika Kombe la Chalenji wakati wa robo fainali dhidi ya wenyeji Ethiopia.

Kerr amesema: “Mkude asahau kupata nafasi ya kupiga penalti katika kikosi changu, mpigaji wangu mkuu wa penalti ni Ibrahim Ajibu.

“Pia mchezaji yeyote wa Simba anaweza kupiga penalti lakini siyo Mkude.” Akaongeza kwa utani akisema, ni bora ampe jukumu hilo mtunza vifaa, Hamis Mtambo.

“Mkude anatakiwa kuwa makini na upigaji wake, kwa sasa hayupo katika orodha yangu ya wapigaji penalti, ila hili ni jambo la muda mfupi tu.”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic