January 23, 2016


Kiungo kinda wa Simba, Said Ndemla, anatarajia kwenda kufanya majaribio kwenye kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo ili kusaka nafasi ya kucheza soka katika klabu hiyo.

Hivi karibuni, Watanzania, Abuu Ubwa na Haruna Chanongo walienda kufanya majaribio Mazembe ambapo kwa sasa hatua iliyobaki ni makubaliano kati yao na Stand United inayowamiliki wachezaji hao.

Jamali Kisongo ambaye ni meneja wa Mbwana Samatta, amesema kuwa, ataendelea kuwasaidia wachezaji wa Tanzania kupenya kwenye soka la kimataifa kama Samatta.

“Nimewapeleka Ubwa na Chanongo kufanya majaribio TP Mazembe, kinachoendelea sasa ni mazungumzo kati ya Stand na Mazembe kwa ajili ya usajili.

“Ndemla naye nitampeleka akafanye majaribio kule, lengo ni kuwasaidia wachezaji wengi wa hapa nyumbani kupata fursa ya kucheza soka nje ya mipaka ya nchi yetu.

“Mbali na Ndemla, pia kiungo wa Mtibwa (Sugar), Mohammed Ibrahim, naye anahitajika kule baada ya awali safari yake kushindikana,” alisema Kisongo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic